Jumatatu, 06 Mei 2013 21:32
>>RVP: “NIMESUBIRI MUDA MREFU KUWA BINGWA!!”
>>ALIHAMA KUSAKA TAJI, SI KUPIGANIA 4 BORA MIAKA NENDA RUDI!
>>KOMBE RASMI OLD TRAFFORD JUMAPILI MEI 12!!

Jumapili, Mei 12, Siku ambayo Man United
watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa BPL, itakuwa ni Wiki 3 tangu Robin
van Persie apige Hetitriki walipoifunga Aston Villa 3-0 na rasmi
kuwatazwa kuwa Mabingwa.
Ushindi huo na Bao hizo za Van Persie
ulikuwa ni uthibitisho rasmi kuwa yeye ndie alikuwa ufunguo wa Man
United kutwaa Taji lao la 20 la Ubingwa na kuzidi kujikita kuwa wao ndio
Klabu Bora England kwa kutwaa Mataji mengi kupita nyingine yeyote.

Van Persie, ambae aliihama Arsenal
mwanzoni mwa Msimu huu ili asake Mataji badala ya kupigania kufuzu 4
Bora Miaka nenda rudi, ametamka: “Ni hisia ambayo huwa unaiota tu! Kila
kitu ni kunyanyua lile Kombe! Tulipigaji Picha safi tulipoifunga Villa
na kutwaa Ubingwa lakini kuna kitu kilikosekana! Ni Kombe!”
Aliongeza: “Hiyo ndio Picha nitaitia
fremu na kuitundika Nyumbani kwangu, mimi nikinyanyua Kombe la Barclays
Premier League! Nashindwa kusubiri muda huo! ”
Wakati akihamia Man United mwanzoni mwa
Msimu kuna baadhi ya Watu walikuwa na wasiwasi na uhamisho huo lakini
kwa Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man United, na Van Persie, kulikuwa
hamna hilo na mwenyewe Van Persie anaeleza: “Nisingehama kama ningekuwa
na mashaka. Tangu Siku ya kwanza nilikuwa nina hakika tutashinda Msimu
huu. Niliona Wachezaji mazoezini. Niliwaona wanavyojituma, wao na
Makocha. Ukichanganya vyote hivyo unapata Timu ya Mabingwa. Kubwa zaidi
ni kuwa pamoja na Timu yenye Wachezaji wanaojua kushinda.”
Mbali ya Kombe la Ubingwa, Van Persie
pia ndie anatarajiwa kutwaa Butu ya Dhahabu kwa kuwa anaongoza akiwa
Mfungaji Bora wa BPL akiwa na Goli 25 na kufuatiwa na Luis Suarez wa
Liverpool, ambae yupo Kifungoni Mechi 10 hivyo hatamletea upinzani, na
anaefuatia ni Gareth Bale ambae yuko Bao 5 nyuma.
Lakini mwenyewe Van Persie anasema:
“Ukweli ni kuwa hiyo Tuzo si sahihi. Haya Magoli ni ya Timu nzima. Bora
wangetoa Kiatu cha Dhahabu kwa Timu! Ingawa itafurahisha kushinda hiyo
lakini Ubingwa ndio muhimu!”
WAFUNGAJI BORA:
NA |
JINA |
TIMU |
GOLI |
1 |
Van Persie |
Man United |
25 |
2 |
Suarez |
Liverpool |
23 |
3 |
Bale |
Tottenham |
20 |
4 |
Benteke |
Aston Villa |
18 |
5 |
Michu |
Swansea |
17 |
6 |
Ba |
Chelsea |
15 |
7 |
Lambert |
Southampton |
14 |
|
Lukaku |
West Brom |
14 |
8 |
Berbatov |
Fulham |
13 |
|
Lampard |
Chelsea |
13 |
|
Walcott |
Arsenal |
13 |
9 |
Cazorla |
Arsenal |
12 |
|
Dzeko |
Man City |
12 |
|
Rooney |
Man Utd |
12 |
10 |
Aguero |
Man City |
11 |
|
Defoe |
Tottenham |
11 |
|
Fellaini |
Everton |
11 |
|
Fletcher |
Sunderland |
11 |
|
Giroud |
Arsenal |
11 |
|
Kone |
Wigan |
11 |
|
Le Fondre |
Reading |
11 |
|
Tevez |
Man City |
11 |
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA
Jumatatu Mei 6
[Saa 4 Usiku]
Sunderland v Stoke
Jumanne Mei 7
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Man City v West Brom
Wigan v Swansea
Jumatano Mei 8
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Tottenham
Jumamosi Mei 11
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea
Jumapili Mei 12
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke v Tottenham
[Saa 11 Jioni]
Everton v West Ham
Fulham v Liverpool
Norwich v West Brom
QPR v Newcastle
Sunderland v Southampton
[Saa 12 Jioni]
Man United v Swansea
Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan
[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City
Jumapili 19 Mei
***MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
**FAHAMU: BINGWA TAYARI NI MANCHESTER UNITED!!
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Man Utd |
36 |
42 |
85 |
2 |
Man City |
35 |
30 |
72 |
3 |
Chelsea |
35 |
34 |
68 |
4 |
Arsenal |
36 |
31 |
67 |
5 |
Tottenham |
35 |
18 |
65 |
6 |
Everton |
36 |
14 |
60 |
7 |
Liverpool |
36 |
25 |
55 |
8 |
West Brom |
35 |
1 |
48 |
9 |
Swansea |
35 |
-1 |
43 |
10 |
West Ham |
36 |
-8 |
43 |
11 |
Stoke |
35 |
-10 |
40 |
12 |
Fulham |
36 |
-11 |
40 |
13 |
Aston Villa |
36 |
-21 |
40 |
14 |
Southampton |
36 |
-11 |
39 |
15 |
Norwich |
36 |
-22 |
38 |
16 |
Newcastle |
36 |
-23 |
38 |
17 |
Sunderland |
35 |
-12 |
37 |
18 |
Wigan |
35 |
-22 |
35 |
19 |
Reading |
36 |
-26 |
28 |
20 |
QPR |
37 |
-29 |
25 |
**QPR & READING TAYARI ZIMESHUKA DARAJA
No comments:
Post a Comment