DAR LIVE 2009 NGWAIR,FID Q AND MZUNGU CHIZI(MUSIC VIDEO)
Thursday, May 30, 2013
Tuesday, May 28, 2013
Saturday, May 25, 2013
Friday, May 24, 2013
FOXY BROWN AKANA KUMTUSI JAY-Z KUWA ANA GONJWA LA ZINAA(NEWS)
Brown anazungumzia ripoti zinazosema,hivi karibuni alienda kwenye baby shower na kuanza kumsema Jay na maisha yake ya kimapenzi kwa mmoja wa wageni katika sherehe hiyo- na kusema kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, na kuwa alipoteza bikira yake kwake wakati alipokuwa na miaka 15 na Jay alikuwa na miaka 27.
kuna mengi yaliyozungumzwa ikiwa ni pamoja na tuhuma za Jay kujihusisha na wizi, video ya ngono na STDs.
Foxy amesema, ripo hizo ni za kijinga kabisa, na nilipoziskia ziliniumiza san atumbo, na kila mmoja aliehusika atapigiwa simu na mwanasheria wangu
Jay siku zote amekuwa ni mtu mzuri kwangu na familia yangu, rafiki mzuri kwa miaka yote hii niliyomfaham, na hatukuwa na chochote zaidi ya mafanikio makubwa kama team
Beyonce, mke wake amekuwa ni mtu mzuri sana kwangu,sitakubali hater yoyote kutengeza story na kuniharibia heshima yangu na muonekano wangu.
huku kuvunjiana heshima hakuweza kuvumilika.
Wednesday, May 22, 2013
NI KIVUMBI TU NDANI YA MTWARA MAENEO YALIYO TARAJIWA KUWEKWA VIWANDA
Mabomu yameapigwa mfululizo Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa.
Eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda likiteketea kwa moto. Eneo liko karibu na bahari. Lilikuwa linamilikwa na serikali na ujenzi chini ya kampuni kutoka Marekani ulikuwa unaendelea. Wazungu wamekusanya baadhi ya vitu vyao na kuondoka eneo hilo.
Zero Brain E03 With Dubo.flv
ZERO BRAIN WITH DUBO JESUS SON(DIR. RINGLE THE DON)
"Nina mistari ya moto ila nnachana mpaka sheli"
Monday, May 20, 2013
AFANDE ASUSA KULA BAADA YA SIMBA KULA KIPIGO

Jumamosi (May 18) kulikuwa na mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga na timu ya Simba iliupoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 2 kwa bila na Yanga.
King Selemani ama Afande Sele kutoka mji kasoro bahari Morogoro ni moja ya watu wanaonekana kuwa ‘addicted’ na ushabiki wa soka kiasi cha kushindwa kuvumilia maumivu ya kufungwa kwa timu anayoishabikia, Simba kitendo kilichompelekea asuse kula toka Jumamosi.
Akizungumza na Suddy Brown katika U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi.pole sana Afande Sele...!!!!!
Monday, May 13, 2013
AFANDE SELE(A.K.A SIMBA DUME) APATA UDHAMINI TOKA KWA ZITO KABWE

Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO. Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.
Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA":
Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA":
Friday, May 10, 2013
Tuesday, May 7, 2013
Monday, May 6, 2013
RVP ANGOJEA KOMBE LA UBINGWA KWA HAMU KUBWA!!
>>RVP: “NIMESUBIRI MUDA MREFU KUWA BINGWA!!”
>>ALIHAMA KUSAKA TAJI, SI KUPIGANIA 4 BORA MIAKA NENDA RUDI!
>>KOMBE RASMI OLD TRAFFORD JUMAPILI MEI 12!!

Jumapili, Mei 12, Siku ambayo Man United
watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa BPL, itakuwa ni Wiki 3 tangu Robin
van Persie apige Hetitriki walipoifunga Aston Villa 3-0 na rasmi
kuwatazwa kuwa Mabingwa.
Ushindi huo na Bao hizo za Van Persie
ulikuwa ni uthibitisho rasmi kuwa yeye ndie alikuwa ufunguo wa Man
United kutwaa Taji lao la 20 la Ubingwa na kuzidi kujikita kuwa wao ndio
Klabu Bora England kwa kutwaa Mataji mengi kupita nyingine yeyote.

Van Persie, ambae aliihama Arsenal
mwanzoni mwa Msimu huu ili asake Mataji badala ya kupigania kufuzu 4
Bora Miaka nenda rudi, ametamka: “Ni hisia ambayo huwa unaiota tu! Kila
kitu ni kunyanyua lile Kombe! Tulipigaji Picha safi tulipoifunga Villa
na kutwaa Ubingwa lakini kuna kitu kilikosekana! Ni Kombe!”
Aliongeza: “Hiyo ndio Picha nitaitia
fremu na kuitundika Nyumbani kwangu, mimi nikinyanyua Kombe la Barclays
Premier League! Nashindwa kusubiri muda huo! ”
Wakati akihamia Man United mwanzoni mwa
Msimu kuna baadhi ya Watu walikuwa na wasiwasi na uhamisho huo lakini
kwa Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man United, na Van Persie, kulikuwa
hamna hilo na mwenyewe Van Persie anaeleza: “Nisingehama kama ningekuwa
na mashaka. Tangu Siku ya kwanza nilikuwa nina hakika tutashinda Msimu
huu. Niliona Wachezaji mazoezini. Niliwaona wanavyojituma, wao na
Makocha. Ukichanganya vyote hivyo unapata Timu ya Mabingwa. Kubwa zaidi
ni kuwa pamoja na Timu yenye Wachezaji wanaojua kushinda.”
Mbali ya Kombe la Ubingwa, Van Persie
pia ndie anatarajiwa kutwaa Butu ya Dhahabu kwa kuwa anaongoza akiwa
Mfungaji Bora wa BPL akiwa na Goli 25 na kufuatiwa na Luis Suarez wa
Liverpool, ambae yupo Kifungoni Mechi 10 hivyo hatamletea upinzani, na
anaefuatia ni Gareth Bale ambae yuko Bao 5 nyuma.
Lakini mwenyewe Van Persie anasema:
“Ukweli ni kuwa hiyo Tuzo si sahihi. Haya Magoli ni ya Timu nzima. Bora
wangetoa Kiatu cha Dhahabu kwa Timu! Ingawa itafurahisha kushinda hiyo
lakini Ubingwa ndio muhimu!”
WAFUNGAJI BORA:
NA |
JINA |
TIMU |
GOLI |
1 |
Van Persie |
Man United |
25 |
2 |
Suarez |
Liverpool |
23 |
3 |
Bale |
Tottenham |
20 |
4 |
Benteke |
Aston Villa |
18 |
5 |
Michu |
Swansea |
17 |
6 |
Ba |
Chelsea |
15 |
7 |
Lambert |
Southampton |
14 |
|
Lukaku |
West Brom |
14 |
8 |
Berbatov |
Fulham |
13 |
|
Lampard |
Chelsea |
13 |
|
Walcott |
Arsenal |
13 |
9 |
Cazorla |
Arsenal |
12 |
|
Dzeko |
Man City |
12 |
|
Rooney |
Man Utd |
12 |
10 |
Aguero |
Man City |
11 |
|
Defoe |
Tottenham |
11 |
|
Fellaini |
Everton |
11 |
|
Fletcher |
Sunderland |
11 |
|
Giroud |
Arsenal |
11 |
|
Kone |
Wigan |
11 |
|
Le Fondre |
Reading |
11 |
|
Tevez |
Man City |
11 |
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA
Jumatatu Mei 6
[Saa 4 Usiku]
Sunderland v Stoke
Jumanne Mei 7
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Man City v West Brom
Wigan v Swansea
Jumatano Mei 8
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Tottenham
Jumamosi Mei 11
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea
Jumapili Mei 12
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke v Tottenham
[Saa 11 Jioni]
Everton v West Ham
Fulham v Liverpool
Norwich v West Brom
QPR v Newcastle
Sunderland v Southampton
[Saa 12 Jioni]
Man United v Swansea
Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan
[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City
Jumapili 19 Mei
***MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
**FAHAMU: BINGWA TAYARI NI MANCHESTER UNITED!!
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Man Utd |
36 |
42 |
85 |
2 |
Man City |
35 |
30 |
72 |
3 |
Chelsea |
35 |
34 |
68 |
4 |
Arsenal |
36 |
31 |
67 |
5 |
Tottenham |
35 |
18 |
65 |
6 |
Everton |
36 |
14 |
60 |
7 |
Liverpool |
36 |
25 |
55 |
8 |
West Brom |
35 |
1 |
48 |
9 |
Swansea |
35 |
-1 |
43 |
10 |
West Ham |
36 |
-8 |
43 |
11 |
Stoke |
35 |
-10 |
40 |
12 |
Fulham |
36 |
-11 |
40 |
13 |
Aston Villa |
36 |
-21 |
40 |
14 |
Southampton |
36 |
-11 |
39 |
15 |
Norwich |
36 |
-22 |
38 |
16 |
Newcastle |
36 |
-23 |
38 |
17 |
Sunderland |
35 |
-12 |
37 |
18 |
Wigan |
35 |
-22 |
35 |
19 |
Reading |
36 |
-26 |
28 |
20 |
QPR |
37 |
-29 |
25 |
**QPR & READING TAYARI ZIMESHUKA DARAJA
CLOUDS WAFUNGUKA KUHUSU JAY DEE
RUGE MUTAHABA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI
wa Clouds Media Group kwa kupitia Mkurugenzi wao wa Utafiti na Matukio,
Ruge Mutahaba, umemtaka msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jay
Dee ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa
kujiegemeza kwa kueneza matusi kwao.
Clouds
Media leo wamefungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi
mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa
wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya
Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwa akirushwa moja kwa moja
katika redio ya Clouds FM, Mutahaba alisema Jay Dee amekuwa akilalamikia
mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na matangazo yake
yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia Sh 240,000.
Alisema
suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa redio yao haiwezi
kukataa matangazo kwakuwa ndiyo wanayowafanya waendelee kuwa kinara
katika suala zima la kuiendesha Clouds FM.
“Nilimwambia
kamwe hatuwezi kukataa matangazo na kama kuna lolote limefanyika, basi
ni kwa bahati mbaya, ukizingatia kuwa tayari alishafanya kazi nyingi
pamoja na kupewa urahisi kwenye kazi zake kwa kupitia Clouds FM.
“Pamoja
na yote hayo, bado matusi na kejeli yaliendelea hasa katika mitandao ya
kijamii jambo lililotufanya tuamuwe sasa kujibu japo hapo kabla
tuliamua kubaki kimya kwa ajili ya kulinda hadhi ya kazi zetu,” alisema.
Kuhusu
shutuma za kuitangaza zaidi Skylight Bendi, Ruge alisema bendi hiyo si
mali ya Joseph Kusaga, Mkurugenzi wao wala yeye, kama madai hayo
yanavyotolewa bila kufanya utafiti, isipokuwa ni mali ya Sebastian
Ndege.
“Kama
kuna mvutano kati ya Machozi Bendi na Skylight basi ni wa kibiashara
maana wote wanalipa fedha za matangazo na kama chanzo ni Jay Dee kuporwa
wanamuziki wake, hilo si jambo geni kwenye muziki.
“Dada
yangu Asha Baraka asingekuwa makini angelia sana, maana kila bendi
inayoanzishwa au kuendeshwa lazima ichukuwe wanamuziki kutoka kwake,
ukizingatia kuwa ni jambo la kawaida hivyo tumuomba Jay Dee atumie
busara katika hili pamoja na kuumiza kichwa kupokea ushindani na
changamoto kama hizo za kuchukuliwa wanamuziki,” aliongeza Ruge.
Aidha,
Ruge alisema Clouds FM ni redio ya watu binafsi, hivyo si ina utaratibu
wake katika utendaji wa kazi, ikiwapo kuchagua nyimbo au kuacha kupiga
kama kuna mtu amekwenda kinyume, hasa wale wanaopita nje na kuanza
kuwatusi, kuwakejeli bila kukumbuka fadhira walizofanyiwa kabla ya kuwa
maarufu wao.
Pia
alisema Clouds FM ipo tayari kufanya majadiliano ya wazi na mtu yoyote
mwenye hisia tofauti juu yao, huku ikiwataka wasanii waongeze bidii
katika kazi zao ili wasimlaumu mtu wanapoanguka na kuwapisha wengine,
maana muziki unaonekana ni wa kupokezana vijiti.
Katika
siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa hasa kwenye
mitandao ya kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo rasmi
kutoka kwa Mwanamuziki Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds
FM na wakurugenzi wake Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
TAARIFA KAMLI YA RUGE HII HAPA
Kwa
mtazamo wangu, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake ingawa
kwenye nchi yetu ya Tanzania, tumezoea maoni hayo kutolewa kwa lugha ya
ustaraabu na staha.
Maoni
kuhusu nani wa kuja kwenye msiba wako au nyimbo za kupigwa kwenye msiba
wako ni haki ya kila mwananchi na hakuna atayeuingilia uamuzi huo.
Maoni pia ya redio gani mtu anaipenda au tv gani pia nayo ni utashi wa
mtu mwenyewe.
Uongozi
wa Clouds FM ulikuwa umefikia maamuzi ya kutojadili jambo hili kutokana
na kuamini kuwa ni tatizo binafsi la mtu na sio jambo lenye maslahi ya
Taifa hivyo kwa uhalali linahitaji majadiliano au mazungumzo binafsi.
Sura
ambayo jambo hili limewekwa na kulifanya kama dharura ya kitaifa sio
sahihi kabisa kutokana na kukosekana na hoja za kina za kuhitaji majibu
na pili kukosekana kwa ujumla wa tija kwa tatizo hili kitaifa.
Bado
ninaamini linatakiwa kubaki kama tatizo la mtu binafsi ila inapofika
taarifa zikapotoshwa kwa nia ya kuwapa mtazamo tofauti wasikilizaji
wetu, Clouds FM inataka kuweka maslahi ya wasikilizaji, wabia wetu wa
biashara na watanzania wote mbele kwa kuwapa taarifa sahihi za jambo
hili.
Clouds
Media Group inapata lawama kubwa sana kutoka kwa watu wengi ambao
pamoja na kuunga mkono ukimya wetu wanajiuliza ni kwanini hatukufanya
jitihada za kumaliza tatizo hili bila kufika hatua iliyofikia sasa ya
matusi, kebehi na vitisho kutwa vinavyoelekezwa kwetu na pia vinaendelea
kuichafua tasnia ya muziki hasa hasa Bongo flava; ambayo imefika mahali
inaonekana kila changamoto inayomkabili msanii wa Bongo flava lazima
itatuliwe kwa njia za mabavu (matusi, vitisho na kuchafuana).
Lawama hizo sio za kweli na
naomba nirudi nyuma kidogo kwenye historia ya jambo hili. Tarehe 14
mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye tweeter account ya Jaydee, alipost
kifuatacho:
Nilichofanya
ni kumpigia simu na kuzungumza nae. Akasema sijaandika kwenye blog
chochote, nikamwambia Jide mi nakuheshimu sana. Nimekupigia kwasababu
naamini kama kuna kitu chochote ni bora nisikie kwako, nategemea na wewe
pia utanipigia iwapo kuna jambo lolote lile. Tulikotoka sisi
hatutakiwi kuendeshwa na majungu na maneno ya mtaani.Hiyo ilikuwa tarehe
14 mwezi December mwaka jana. Baada ya kama dk 10 hivi akanitumia msg (
ambazo bahati nzuri nilizihifadhi) na kusema ni kweli alikuwa
ananizungumzia mimi kwa sababu kuna vitu kadhaa vinamsumbua na aliambiwa
mimi ndo nilihusika navyo.
La
kwanza, ‘nililipa matangazo ya shs laki mbili na 40 ila hayajachezwa na
wala sijarudishiwa hela yangu, nimeambiwa umekataza matangazo yangu ya
Nyumbani lounge yasipigwe’.
La pili, naruhusu watangazaji wangu wamtukane ikiwa ni pamoja na kupromote zaidi bendi ya Skylight.
Pamoja na kwamba yeye alinitumia message, mimi nilimpigia simu na kumpa ufafanuzi wa yote hayo niliyosema hapo juu.
Nikasema, Biashara
yetu sisi ni matangazo…..kwanini tukataze matangazo yako yasipigwe??
Labda bahati mbaya tu, jamaa anayebook matangazo alipitiwa kuyabook
kibinadamu ila Gadna si anakuja hapa kila wakati, kwann asimkumbushe
tu?? Tutayasogeza tu mbele hadi wiki inayofuata, kwanini niyakataze
wakati muda sio mrefu tumetoka kuleta biashara ya Repa bora wa bendi
hapo hapo Nyumbani lounge.
Niliendelea kujibu kuwa
sio kweli kabisa, siwezi kuruhusu jambo kama hilo na kama ni kweli
mtangazaji anamtukana anifahamishe ni nani na kwenye kipindi gani,
nitasikiliza kipindi na kama ni kweli nitamfukuza kazi ( Clouds ina
mitambo ya kuhifadhi matangazo yake yote kwa takribani miezi 9).
Hili
nilimjibu kwa kirefu kidogo ikiwemo kumwambia akaze buti maana Skylight
Band wanakuja juu nk nk. (Skylight Band ni bendi inayofanya vizuri sana
hapa mjini na ilipoanza ilichukua baadhi ya majina makubwa kutoka
Machozi Band).
Baada ya kumaliza mazungumzo tuliagana vizuri tu kwa miadi ya kukutana nikirudi maana nilikuwa safarini.
Kwahiyo
ukiniuliza Jaydee anacholalamika ni nini??? Jibu langu litakuwa ni hayo
mambo mawili maana hata nyie watanzania wenzangu mnaosoma mitandao ya
kijamii mtakubaliana na mimi kuwa amekuwa anashambulia personality zetu,
mimi na Mkurugenzi mwenzangu bila kuweka wazi hoja za msingi kuhusu
yale anayotutuhumu nayo. Nimejitahidi sana kuelewa tatizo lake hasa ni
nini na imekuwa inanipa shida kidogo?? Nimejitahidi sana kufikiria ni
mirija ipi ya biashara kwake imeingiliwa, nakosa majibu???
Clouds
FM ni ya watu na watu wanaweza kufanya makosa kweli na hata kusababisha
matangazo ya laki 2 na 40 yasirushwe, kwa hilo nilishazungumza na
Jaydee na kuomba radhi toka tarehe 14 December 2012. Clouds FM haina
ubia wowote ule na Skylight Band (ni bendi iliyoanzishwa na
Mtanzania)hivyo kuipromote ni katika misingi ile ile ya biashara kama
tunavyopromote bendi yeyote ile na vilevile Clouds FM pia haihusiki
kabisa na kutetereka kwa biashara ya chakula, vinywaji na bendi
inayofanyika Nyumbani lounge. Inashangaza hata kuhusishwa na biashara ya
Nyumbani lounge…!!!
Sina
ugomvi binafsi na Jaydee wala Gadna, na tarehe 12 February mwaka huu,
nilienda kuazima stools kwa ajili ya shooting kutoka kwenye sehemu yao
ya biashara ingawa yeye amekiri kuwa na ugomvi mkubwa na sisi binafsi na
Clouds kama chombo.
Nyimbo
yake iliyotoka ya Joto Hasira ilipokelewa vizuri sana kulinganisha na
nyimbo mbili zilizopita ‘Yeye’ na ‘Mimi ni mimi’ ambazo hazikufanya
vizuri pamoja na jitihada kubwa ya kuzipromote. Joto Hasira iliacha
kupigwa kutokana na shinikizo lake mwenyewe, ikiwa imeshachezwa mara 48
ndani ya wiki tatu toka imetoka wote tulipigwa na bumbuwazi na kujiuliza
ni kitu gani tumefanya kuambiwa hatupigi nyimbo na lawama nyingine.
Kama ofisi tukaona tukae kimya na kusubiri hatua inayofuata ukizingatia
tuliendea kupiga nyimbo na video hata baada ya maneno makali ya mwanzo.
Kauli haikubadilika, mbaya zaidi kauli za kebehi na kuchafuana
zikaongezeka hadi kufikia uamuzi wa sisi kama taasisi kuamua rasmi
kutopiga nyimbo zake hadi atakapofuta kauli zake na kuomba msamaha.
Kupiga
au kutopiga nyimbo kwa kituo cha redio ni jambo la kawaida na kwasababu
ni chombo binafsi ni muhimu kwa watu kama Jaydee na wasanii wengine (na
hata wananchi wa kawaida) kuelewa kuwa kila ofisi ina taratibu zake na
iwapo utatokea ukiukaji wa taratibu hizo, policy ndo zinaongoza
maamuzi. Hebu tujiulize, mbona sio mjadala wa Taifa msanii Diamond
hapigwi karibu miezi sita sasa kwenye station ya Magic FM, Ray C na Ali
Kiba kwa karibu mwaka mzima walikuwa nyimbo zao na video hazipigwi na
East Africa hadi walipoomba msamaha, hadi Yanga kwa muda mrefu walikuwa
hawatangazwi habari zao kwenye chombo kimoja cha habari. Hayo ni mambo
ya ofisi binafsi na hakuna anayeweza kulaumu maamuzi hayo.
‘Management
reserves the right of admission’……nani hajaona kibao hiki kwenye hoteli
nyingi tu nchini, nani asiyefahamu kuwa kuna hoteli ambazo ukienda kama
mwanamke peke yako unakataliwa? Hizi ni taratibu na kila mahali
zipo…..hata nyumbani lounge ndo maana Sam Machozi ambaye yuko Skylight
Band zamani alikuwa mwanamuziki wa Machozi Band amepigwa marufuku pale
Nyumbani lounge na halalamiki maana ni sehemu binafsi na ina taratibu
zake. Ni tofauti na sehemu za wazi za umma kama Mnazi mmoja au kituo cha
basi cha Magomeni.
Clouds
Media Group inafuata taratibu zote za nchi na za kimkoa ila na yenyewe
pia inaweka taratibu zake za uendeshaji. Sasa isifike mahali Clouds
inapoweka taratibu zake hizo na kuzitekeleza inaonekana inafanya makosa. Yaani hata tarehe za kufanya show nchi hii tunatakiwa kupeleka maombi sehemu ili watu zaidi ya mmoja wasifanye show kweli??? Kwanini
tunachanganya ushindani na fitina…..acha ziwepo bendi 10
zinazoshindana, kuanzishwa kwa bendi nyingine kusiangaliwe kama fitna. Na hata mtu akianzisha bendi kwa kuchukua wanamuziki kutoka kwenye bendi nyingine, si ndio dhana ya ushindani???
Kama
ni kulalamika kuanzishwa kwa bendi nyingine au kuchukuliwa wanamuziki,
Dadaangu Asha Baraka si angeshafanya maandamano nchi nzima. Ila wote
tunatambua kuwa ni jasiri ndo maana anatulia na kuanza upya.
Mbona
watu hawalalamiki baa zinapofunguliwa 10 mtaa mmoja, au saloon za
nywele, moja jirani na nyingine. Ni lazima tukubali na tuzoea ushindani.
Pamoja
na ushindani kingine ninachoomba kuwasihi watanzania wenzangu hasa
hasa wasanii wetu zaidi ni kuwa kila mtu na kila kitu kina ‘shelf
life’. Watu wa zamani naamini wanamkumbuka Power Mabula….alikuwa
anatisha sana wakati ule. Au nani anaweza kusahau umaarufu wa Mzee
Nobert Chenga na Kundi la Muungano cultural troupe au labda huko ni
nyuma sana; nani anamkumbuka Kanda Bongo Man, alicharge laki moja enzi
hizooo….au labda hapa katikati umaarufu wa Muumini, Mr Nice au mtu kama
Saida Karoli (alijaza Stadium). Wote hao walikuwa maarufu sana. Sasa
wasanii hawa na wengine wanaokuja wasipojiandaa kuelewa kuwa kila kitu
kina muda wake, tutakuwa na taifa la vijana ambao asubuhi mpaka jioni
badala ya kuhangaikia fursa nyingi zilizopo wataishia kutafuta mtu wa
kumlaumu.
Ni
lazima Edibily Lunyamila atarithiwa sehemu yake na kina Mrisho Ngassa
ambaye naye muda utapita ni lazima atawaachia kina Simon Msuva. Wapo
watu kama kina Dully Sykes walioanza kujiandaa kwa kuwaachia kina
Diamond na wao kufungua studio na kuwa maproducer. Suala la kupokezana
vijiti halikwepeki kuanzia makazini, mpirani na hata kwenye sanaa. Cha
kufanya ni kujiandaa kwa maisha yako baada ya kugawa kijiti chako.
Taarifa
za kutaka kuua muziki wa Bongo flava kwa makusudi zinashangaza, ili
iweje sasa??? Clouds inategemea matangazo ya biashara kama asilimia 95
ya mrija wa mapato na muziki tunaopiga redioni ni sehemu ya maudhui
kwahiyo hakuna namna yeyote ile tutataka muziki huo upotee. Tunafanya
juhudi zote hizi kwasababu tunahitaji nyimbo bora na wasanii bora ili
tuweze kuendelea kuwa kituo bora cha redio.
SUMMARY YA MSIMAMO WETU
Fursa:
Uganda endorsment
TZ ringtones
Album sales – Kina Mamu.
DVD live performance shows.
Meeting ya wasanii wote watoe maoni.
Saturday, May 4, 2013
MATOKEO KIDATO CHA NNE YAFUTWA NA KUSAHISHWA UPYA:
Habari leo hii kutoka bungeni zinaweza kuwa ni sehem nzuri ama habari nzuri kwa wanafunzi wengu huku baadhi wakiona kama ni mizinguo..
sababu inayonifanya kusema hiki, ni pale nilipowafikiria wale waliopata division 1, hofu itakua imetanda baada ya kauli ya wabunge walioteuliwa kufatilia ishu ya kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2011 / 2012, ambapo inaonekana kabisa kurudiwa kusahihishwa upya kwa mitihani hiyo
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne imesomwa bungeni leo na Mh.Lukuvi.
Mh.Lukuvi. amesema sababu zilizosababisha wanafunzi wafeli ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa baraza la mitihani uliotumika bila kuwashirikisha wadau wa elimu
Mh.LukuviI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS.
Hivyo basi, matokeo hayo yamefutwa na yatasahihishwa upya
Subscribe to:
Posts (Atom)